• English
  • Español
  • Kiswahili
Tungependa kusikia maoni yako!

Norton Healthcare inashirikiana na Goodwill Industries of Kentucky Inc. kubadilisha sehemu ya 28th Street na Broadway kuwa Kituo cha Jamii. Hii inajumuisha kujenga hospitali mpya eneo la West Louisville. Hii itakuwa hospitali ya kwanza kufunguliwa kwenye eneo hilo katika zaidi ya miaka 150.

Watu wote katika kila eneo wanapaswa kuwa na fursa sawa za kupata huduma ya afya wanayostahili. Norton Healthcare ilihudumia takriban asilimia 60 ya wakaazi wa West Louisville mwaka wa 2021. Wakaazi wa West Louisville walitembelea hospitali za Norton Healthcare zaidi ya mara 45,000 mwaka jana kupokea matibabu ya wagonjwa wasiolazwa. Tunashirikiana na watoa huduma za afya, familia na viongozi wa eneo ili kutoa huduma kwa watu wote.

Kwa kushiriki katika utafiti huu, maoni yako yatasaidia kuhakikisha kuwa hospitali mpya itashughulikia mahitaji ya jamii. Mwishoni mwa utafiti huu, tafadhali tueleze huduma ambazo ungependa zipatikane kwenye hospitali hii. Utafiti huu utachukua muda mfupi kukamilisha. Pata taarifa kuhusu kituo hiki kwa kutembelea WestLouisvilleHospital.org. Kwenye tovuti hii, unaweza pia kujiandikisha ili upokee taarifa mtandaoni kuhusu hali ya hospitali.

Utafiti huu ni wa siri kabisa. Maelezo utakayotoa yatatumiwa na Norton Healthcare pekee kwa madhumuni ya matayarisho ya hospitali hii mpya. Baada ya kukamilisha utafiti huu, hutapokea majibu yoyote moja kwa moja wala hutapokea barua pepe kutoka Norton Healthcare kuhusiana na utafiti, isipokuwa iwe umejiandikisha kupokea taarifa kuhusu hospitali hii. ASANTE kwa mchango wako!
 
8% of survey complete.

T