Bodi ya Elimu ya Rockford Public Schools (RPS) imeanza kutafuta Msimamizi wake mtarajiwa. Ni muhimu msimamizi atakayefaulu awe mtu aliye na mseto wa sifa, uzoefu, ujuzi wa uongozi na sifa za kibinafsi ambazo walimu, wazazi, wasimamizi na wanafunzi wanatarajia na kuthamini.
Kama sehemu ya utaratibu huu, tunaomba mchango wako wa kusaidia kubuni wasifu wa uongozi unaobainisha sifa za kitaalamu na za kibinafsi zinazotakikana ili kufaulu katika jukumu hili. Wasifu huu utachapishwa kama sehemu ya tangazo la kazi na kutumiwa na Bodi ya Elimu kutathmini waombaji. Wasifu huu ni zana muhimu. Tafadhali toa maoni yako kwa kujaza utafiti ulio hapa chini kabla ya saa sita usiku mnamo Oktoba 2, 2025. Majibu yote hayamtambulishi mhusika. Asante kwa kujaza utafiti huu na kusaidia katika jukumu hili muhimu sana.
Kwa maswali yanayokuomba hasa uchague vitu vitatu (swali la 3, 4, 5, na 7), hakikisha umechagua angalau kitu kimoja lakini si zaidi ya vitatu au hutaweza kusonga kwa swali linalofuata.