MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA)


DODOSO LA KUKUSANYA MAONI KUHUSU KUANDAA KANUNI NDOGO ZA VIFURUSHI, OFA NA PROMOSHENI KATIKA HUDUMA ZA MAWASILIANO YA SIMU

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano kuhusu namna vifurushi vya huduma za mawasiliano zinavyopangwa na kutolewa kwa watumiaji.

Ili kuhakikisha ufanisi na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora kulingana na thamani ya pesa kwa malipo yaliyofanywa na wanaojiunga na vifurushi husika, TCRA imeandaa dodoso hii ili kupata maoni yako na kuyafanyia kazi ipasavyo. Hivyo, tunakuomba utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote katika dodoso ifuatayo na tunakuhakikishia kwamba majibu yako yatakuwa ni siri kati yako na TCRA na yatatumika kwa shughuli za Mamlaka tu.
1.Muda wa ofa na huduma za vifurushi


Unapendekeza vifurushi viwe na muda gani wa chini kabisa na muda
gani wa juu kabisa? (mfano, siku, wiki, mwezi, nk.,)
(Yanahitajika.)
2.Masuala ya gharama na tozo zinazohusu kutozwa zaidi,
kuunganishwa kwenye huduma ambayo haitolewi baada ya kumalizika kwa ghafla kwa uniti za vifurushi.

Je, utaratibu gani uwekwe kuwafidia watumiaji ambao
wamethibitishwa kwamba wametozwa zaidi?
(Yanahitajika.)
3.Ni utaratibu upi utumike kuhakiki utozaji na matumizi ya uniti katika kifurushi?(Yanahitajika.)
4.Ni mfumo gani uwekwe kushughulikia kutozwa zaidi na kumalizika kusikotegemewa kwa vifurushi (hasa vya huduma za data)?(Yanahitajika.)
5.Kuunganishwa kwenye kifurushi bila ridhaa ya mtumiaji

Mfumo gani uwekwe kuwezesha kufikisha ujumbe kwa njia
itakayohakikisha uwazi, kuondoa mzigo kwa mtumiaji na kuhifadhi ushahidi wa kujiunga?
(Yanahitajika.)
6.Huduma zipi mtumiaji aendelee kuzipata kutoka kwa Mtoa Huduma iwapo kifurushi alichojiunga nacho kimemalizika na mtumiaji hajajiunga na huduma za ziada? Huduma hizo ni kama vile kuweza kufanya mawasiliano ya dharura, nk..(Yanahitajika.)
7.Kuwepo usawa juu ya namna ya kupata huduma kwenye vifurushi

Je unashauri kuwe na namba moja itakayotumiwa na wote kupata
taarifa kuhusu vifurushi na huduma nyingine ambazo zinafanana kwa
mitandao yote?

(Yanahitajika.)
8.Kuna haja ya kuwa na jina moja litakalotumika kwa watoa huduma
wote kwa vifurushi visivyokuwa na muda wa mwisho wa matumizi?
(Yanahitajika.)
9.Vipimo vitakavyotumika kufuatilia huduma na bidhaa kwenye
vifurushi.

Unapendekeza nini kuhusu vigezo vya vipimo na tofauti ambazo
zinaruhusiwa/zinakubalika wakati wa kuhakiki matumizi halisi
kulinganisha na uniti zilizonunuliwa au mtumiaji alizolipia alipojiunga
ili haya yazingatiwe wakati wa kuchukua hatua za kiusimamizi?
(Yanahitajika.)
10.Vigezo na Masharti ya huduma kwa njia ya vifurushi

Unasoma kwa kina na kuelewa vigezo na masharti ya kifurushi
kaba ya kununua?
(Yanahitajika.)
11.Vigezo na masharti vinaeleweka na vinatoa taarifa zote
zinazohitajika kufanya uamuzi wenye mantiki?
(Yanahitajika.)
12.Tafadhali andika vigezo na masharti kwenye kifurushi, matangazo
ya huduma na ofa maalum ambavyo unadhani haviko wazi na
vinaleta mkanganyiko na vinatakiwa kuondolewa/kurekebishwa
mara moja.

(Yanahitajika.)
13.Utaratibu gani utumike kuhakikisha watuamiaji wanasoma na
kuelewa, pamoja na kukubali vigezo na masharti ya huduma za
vifurushi?
(Yanahitajika.)
14.Maoni yako kuhusu kupungua kwa ubora wa huduma ikiwemo spidi ya data kadiri kifurushi kinapokaribia kuisha.(Yanahitajika.)
15.Idadi ya vifurushi na aina wanazoweza kuchagua watumiaji


Je unashauri kuwe na kiwango cha mwisho cha idadi ya vifurushi
ambavyo ni rahisi kupatikana na kupitiwa na mtumiaji kabla ya
kuamua kujiunga?
(Yanahitajika.)
16.Unapendekeza vifurushi vingapi kwa kila mtoa huduma?(Yanahitajika.)
17.Kifurushi kiendelee kutumika kwa muda gani kabla ya kuboreshwa
(kurekebisha bei au kiasi cha uniti katika kifurushi)?
(Yanahitajika.)
18.Ni njia ipi bora ya kuwasilisha kwa mtumiaji gharama za matumizi ya vifurushi na taarifa za Vigezo na Masharti kuhusiana navyo?(Yanahitajika.)
19.Idadi ya marudio ya matangazo, ofa maalum na kubadili gharama za vifurushi.

Nini maoni yako kuhusu idadi inayofaa ya matangazo ya huduma na ofa maalum kwa watumiaji?
(Yanahitajika.)
20.Nini maoni yako kuhusu idadi ya marudio ya matangazo ya huduma na ofa maalum kwa watumiaji?(Yanahitajika.)
21.Uelewa kuhusu matumizi ya vifurushi.

Nini maoni yako kuhusu watumiaji kupewa taarifa vifurushi vikifikia asimilia 90 na 100 ya kumalizika kwa kifurushi au wapewe taarifa za huduma zilizobakia (muda wa maongezi, meseji na data) lakini watahadharishwe angalau mara mbili kabla ya asimilia 100 ya matumizi.
(Yanahitajika.)
22.Kumalizika kwa vifurushi na kupeleka mbele vifurushi
visivyotumika.

Ni zipi athari za uamuzi huu kwenye kupanga bei na matumizi ya huduma za mawasiliano ya simu?
(Yanahitajika.)
23.Nini maoni yako kuhusu kuwepo kwa vifurushi ambavyo havina muda wa kumalizika?(Yanahitajika.)
24.Nini mapendekezo yako, ikiwa ni pamoja na Vigezo na Masharti ya kupeleka mbele data?(Yanahitajika.)
25.Nini mapendekezo yako, ikiwa ni pamoja na Vigezo na Masharti ya kuhamisha data kutoka mtumiaji mmoja kwenda mwingine katika mtandao huohuo?(Yanahitajika.)
26.Kuwepo kwa Sera ya Matumizi ya Haki (Fair use Policy)
kuwawezesha watumiaji kuwa na taarifa muhimu kusimamia na
kufuatilia matumizi.

Kwa upande wa kuwepo kwa Sera ya Matumizi ya Haki kuhusiana na utangazaji wa huduma, ofa na vifurushi; je viwango vya Sera ya Matumizi ya Haki itakayotolewa kwa watumiaji viweje ili watumiaji waendelee kuwezeshwa kufanya uamuzi baada ya kuwa na taarifa muhimu?
(Yanahitajika.)
27.Viwango vya Sera ya Matumizi ya Haki kuhusiana na matumizi ya
vifurushi viweje?
(Yanahitajika.)
Hatua Iliyopigwa Kwa Sasa,
0 kati ya 27 yamejibiwa