Kutokana na upungufu wa mahudhurio ni lazima kudumisha umbali wa futi sita (6) kimwili, katika madarasa na mabasi. Shule zetu zina mipango ya kutoa mafunzo kwa kutumia mseto wa ratiba ya shule na kujifunza nyumbani. Hata hivyo, njia ya msingi ya mafunzo itafanyika kwa mbali kutumia nyenzo za kujifunza mtandaoni za RCPS. Kama/wakati mwongozo kutoka Idara ya Afya ya Virginia (VDH) inaruhusu ongezeko la uwezo, wanafunzi wataweza kuhudhuria shule mara zaidi.
Wataalamu wa Afya ya Umma wamefanya wazi kuwa haiwezekani kuwa na mazingira yasiyo ya hatari wakati wa janga la kimataifa. Tumejitahidi kupea kila familia na chaguo kulingana na kiwango cha hatari wanachagua. Tunatarajia kwamba baadhi ya familia zitasita kutuma wanafunzi wao kwenda shule hadi kuwe na chanjo cha COVID-19 na/au hadi matibabu yaliyo idhinishwa kupatikana. RCPS itatoa fursa ya kujifunza kwa umbali kwa familia ambazo zitachagua hatari ya chini.
Tunaelewa maoni yako yanaweza kubadilika baada ya muda, kwa hivyo maswali yafuatayo yanalenga tu kuchukua hisia yako kwa wakati. Majibu yako hayata athiri uwezo wako wa kujiandikisha katika RCPS.